Utafiti: Kumshika mkono unayempenda akiwa anaumwa kunapunguza maumivu


Wanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Colorado, Marekani wamesema kuwa kumshika mkono mtu unayempenda wakati anahisi maumivu kunasaidia kupunguza hali ya maumivu kwa zaidi ya 60%, kwa mujibu wa utafiti wao.

Utafiti umeonesha kuwa wanawake wengi waliofanyiwa upasuaji au wakati wa kujifungua hupunguza mawimbi ya maumivu yatokayo kwenye ubongo kwenda kwenye mwili iwapo walishikwa mikono na waume zao.

Dr Pavel Goldstein, akielezea hali hiyo inavyoweza kutokea kisayansi amesema cingulate cortexambayo ni sehemu ya ubongo huchelewa kutuma taarifa kwenye ubongo kuhusu kuwepo kwa maumivu kutokana na uwepo wa homoni ya Oxytocin inayozalishwa iwapo mtu atashikana mikono na mtu wanayependana.

Utafiti pia umeonesha moyo hupungua mapigo na kuwa ya kawaida wakati wa maumivu makali kutokana na saikolojia ya binadamu kujisikia amani anapokuwa na mtu anayempenda wakati wa kuumwa. Hivyo, imeonekana ni muhimu kwa wanaume kuwashika mikono wake zao wakati wa kujifungua.

Toa Comment: Baada ya kusoma hii tunaomba tuachie maoni yako ili tupate mawazo yako kuhusu mada husika. Contact Us
Related Posts
COMMENT