Zawadi Iliyo Nzuri Kupita Zote Siku ya Valentine

Wachunguzi wameona mbinu nzuri ya kuongeza mapenzi ili kuwa na valentine nzuri.

Mwaka uliopita huenda mkeo au mumeo alikupa zawadi nzuri ya valentine iliokuwa ya kipekee.

Kwa kufuatilia mila zetu za Kiafrika zawadi zetu ni za aina mbalimbali ,hereni ,saa, mikufu , wengine hata nguo ,kila mtu na wazo lake wengine hununua kadi, maua.

Hivyo vitu vinaonyesha mapenzi kwa kila mmoja wenu ? Ni muhimu sana ya kwamba zawadi hizo zitamfanya mtu mwingine ajisikie kupendwa na kuwa na furaha na afya. Au ni kuiga mila za watu wengine tu ?

Badala ya hivyo vitu ambavyo huwa tunaahidiana kupeana kama zawadi, kwa nini visiwepo na vingine ambavyo vinasaidia akili zetu na miili yetu, na ulimwengu mzima, kwa kujitolea kusaidia wengine wenye mahitaji muhimu. Hasa wajane kweli, watoto yatima.

Siku hio ni ya kutafuta watu ambao wanatakiwa kujisikia na wao wanapendwa na kujaliwa na watu, pesa ambayo unataka kununulia nguo ya thamani kwa ajili ya kuonyesha upendo kwa mpenzi wako, kwa nini usimwambie mpenzi wako , mume, mke muende kuwaona wagonjwa hospitalini na kuwapa faraja, au kuomba Mungu awape ufahamu wa kutambua ni wapi wenye mahitaji ya kweli.

Furaha watakayopata wao, ndio furaha yenu kubwa kuliko hata kwenda kwenye mahoteli makubwa kutumia hio pesa.

Kutoa kwa namna hio unapunguza blood pressure, ambayo haiwezi kutokea kwa wale ambao wanatumia pesa wenyewe.

Kwa hio hili ni pendekezo na ni jaribio. Kwa siku ya valentine tutoe upendo na sadaka kwa majina ya watu wengine. Kwa kiasi kile kile cha pesa utapata zaidi kwa njia hii, tunaweza kupata furaha na afya ya mahusiano yetu na kusaidia watu kwa wakati huo huo, kuongeza matumizi ya pesa hizo hizo, tunaweza kuimarisha mahusiano yetu. Utaua ndege watatu kwa jiwe moja.

Kwa hio tuwe na maamuzi ya kutoa vizuri, na maisha ambao unaweza kuyaponya, kitu ambacho kinaleta athari inayoonyesha utoaji wa uelewa. Na upendo uwe na thamani .

Naamini utakuwa na furaha kwa ajili ya zawadi hizo za ukomavu wa akili. Ni nzuri kuliko kupeana chokuleti au vinywaji baridi. Tena ni vizuri kama mtasaidiana kutoa hizo zawadi, mtajisikia vizuri kufanya hivyo kusaidia wengine. Mtakuwa mmeamua kubadilisha uzoefu wa mila mpya kwa ajili ya familia zenu.

Itakuwa ni siku ya upendo wa mapenzi ya valentine ambayo haijawahi kutokea katika maisha yenu. Na itawafanya mtambue kuwa ni jinsi gani valentine imefanyika kwa ajili yenu na watu wote wanaowazunguka na hata ulimwengu. Hii yote inatokana na maongezi ambayo yataonyesha upendo wa kweli kwa mwenza wako kwa kuboresha afya yake na furaha yake, pamoja na kuimarika zaidi. Kuna sababu yeyote hapo inayozuia kupata muda wa mazungumzo hayo ?

Share na marafiki wajifunze pia.

Toa Comment: Baada ya kusoma hii tunaomba tuachie maoni yako ili tupate mawazo yako kuhusu mada husika. Contact Us
Related Posts
COMMENT