Njia 5 Akili Yako Imekudanganya Wakati Ulipovunjwa Moyo na Mapenzi


Ulipovunjwa moyo Akili yako ilikutaka uwe unakumbuka maumivu tu kila wakati.

Maumivu ya hisia ambayo yanatokana na kuvunjika moyo yanasababisha magonjwa makubwa yasiotibika. Kwenye hatua hii huwa hakuna mtu anayehusika, wala kitu chochote.

Wewe mwenyewe unaweza kuzika kazi hiyo , kwa kufikiri, au kwa kuondoka mahali unapoumizwa na kwenda mahali salama kwa muda kwanza. Wakati huo sio vizuri kukaa peke yako kwa kuwa kama utabaki mwenyewe, kila unachoona ni yule mtu aliyekuumiza moyo na kusikia maumivu makali zaidi.

Kitu tunachokihitaji zaidi ni maumivu kutulia au yaondoke kabisa, Lakini hiki sicho ambacho akili zetu hukitaka.

Unapokuwa umevunjika moyo , Akili inakuwa na Agenda tofauti na unachotaka kufanya, matokeo yake huishia kukudanganya na kuyafanya mambo yote kuwa mabaya zaidi.

Kama tukitaka kuepuka na kuachana na maumivu ili tusonge mbele , tunahitaji kufahamu ni wakati gani sio wa Kuamini kile ambacho akili inakuambia.

Kwa Nini Tusiamini Akili zetu Tunapokuwa kwenye Maumivu Ya moyo.

Ili usiumie ni vizuri kama utakubali matokeo ya kuvunjwa moyo na mtu uliempenda na kuwa na juhudi ya kusonga mbele. Punguza muda uliokuwa unatumia kumfikiria mtu huyo. kwenye mawazo yako hakikisha unamfuta kidogo kidogo sio mara moja.

Akili huwa inataka kufanya kitu tofauti, mambo kinyume, inataka umfikirie mtu muda wote, ushikilie maumivu bila ya kusahau nani na kilichosababisha ni kitu gani. Akili inapenda kufikiri hivyo kwa kuwa mara nyingi inataka kukulinda. Mfano kama maumivu yalisababishwa na moto wa mkaa, akili itakukumbusha maumivu ya huo moto, kwamba usiguse tena, kuhakikisha unakumbuka jinsi gani maumivu yalikuwa makali. Kwa hiyo akili inafanya kazi ya kukulinda ili usifanye makosa hayo tena. Ni vile vile kwenye maumivu ya kuvunjwa moyo, akili itakukumbusha kila mara ili ufikirie zaidi.

Utakuwa ni mtu wa kufikiria kwamba:

1.Huyo mtu alikuwa bora, hakuna mwingine, hutapata kama yeye.
Utakuwa unakumbuka sifa zake nzuri, mwonekano wake . Hivi vitu vitakuwa vinacheza akilini mwako na kusababisha maumivu makali yasioisha.

2. Mahusiano yalikufanya uwe na furaha kila wakati.

Hapana sio mahusiano , inawezekana ni wewe ulitengeneza hio furaha.

3. Kama ukimpigia simu au kumwandikia ujumbe utajisikia vizuri.

Unakuwa unajiuliza, nipige au nisipige, nimtumie ujumbe au email, vitu hivi vinakuja kwa nguvu. Lakini kumbuka kufanya hivi vitu unaonekana umechanganyikiwa naye na ni muhitaji, utajiumiza mwenyewe.

4. Akili itakuambia kuwa , kuongea na marafiki kuhusu ex wako utapunguza maumivu.

Hapana . hutapunguza. kuongelea hisia za matukio ya maumivu ni kawaida. tena inafaa. kama utafanya hivyo kwa ajili ya kutatua tatizo, au kama unafanya hivyo ili kuthibitisha hisia . Lakini kama utaenda moja kwa moja kuhusu tatizo lako utakutana na maumivu makubwa zaidi.

5. Ni lazima kujua kwa uhakika kwa nini hicho kitu kimetokea.
Kuwa na uelewa kwamba kwa nini hili tatizo limetokea inasaidia .Ingawa , Ni wachache tu ambao wanakuwa wazi na waaminifu kuelezea kitu hicho. Kujaribu kuingia kwenye vichwa vya maex wetu ili kuelewa kwa nini vitu hivi havikufanya kazi ni shimo la panya. Ni bora kutambua na kufahamu kuwa Hawakuwa na upendo au haikuwa chaguo lao, au makosa yamefanyika.

Kubali matokeo ili upone.

SHARE NA MARAFIKI PIA.

Toa Comment: Baada ya kusoma hii tunaomba tuachie maoni yako ili tupate mawazo yako kuhusu mada husika. Contact Us
Related Posts
COMMENT