Dalili 20 Zinazoashiria Kwamba Mapenzi Yenu Yatadumu.

Watu wengi wanakuwa kwenye wasiwasi wa kuachwa au kuvunjika kwa mapenzi yao wakiwa mwanzoni mwa uhusiano au ndoa. Pengine ni kwa sababu wanaona walikuwa wakiwaficha wenza wao baadhi ya vitu ambavyo sasa kwakuwa watakuwa pamoja muda mrefu, hofu ya mwenza kuja kugundua mambo yaliyokuwa yanafichwa inakuwa kubwa na kufanya ushindwe kujua hatua atakayechukua baada ya hapo.

Hata hivyo, wengine wanakuwa na hofu tu si kwa sababu walikuwa wanaficha chochote, bali ni kutokana na kuanza maisha mapya na mtu mwingine, jambo linaloleta wasiwasi endapo utamfaa mwenza wako au kama yeye atakufaa kadhalika.

Zifuatazo ni dalili kwamba wewe na mpenzi wako mtadumu kwenye mahusiano yenu:

1. Tabia ya kila mmoja inatosheleza mapungufu ya mwenzake vizuri kabisa, na kila mmoja anamfanya mwenzake kuwa bora zaidi kwa kuwa pamoja, kila mmoja anakuwa bora zaidi ya anavyokuwa akiwa peke yake.

2. Mnathaminiana na kila mmoja anajali mambo anayoyapenda mwenzake.

3. Mnakuwa na maelewano mazuri kama marafiki tu, bila kulazimisha hali hiyo. Hata inapotokea kutoelewana kati yenu juu ya jambo fulani, kutoelewana huko kunachukuliwa ni kama kila mmoja anataka jambo hilo hilo ambalo ni kumfanya mwenzie awe na furaha.

4. Mnaweza kuongea tu na kutaniana kila mmoja akaridhika na kufurahia kwa kufanya hivyo.

5. Vitu au mambo ambayo anayathamini mwenzio yanafanana na unayoyathamini wewe na mna imani moja mnayoisimamia.

6. Mambo yanayowapa furaha yanafanana au yanakaribiana, na pia anamfanya mwenzake ajifunze mambo mapya ambayo hakuwa akiyafanya kabla.

7. Mitazamo yenu haikinzani mnapojadili mambo ya msingi, lakini pia kila mmoja anakuwa wazi kujadili mawazo mapya yanayofata kudumisha uhusiano.

8. Kila mmoja humfanya mwenzake acheke na kufurahia, bila hata kujaribu.

9. Hamna sababu inayomfanya mwenzako akukasirikie kwa zaidi ya saa moja… kama mkikasirikiana.

10. Mnaaminiana. Hata ikitokea kila mmoja akawa na hofu juu ya mwenzie, bado unakuwa na imani kuwa mwenzako ni mtu unayeweza kumuamini bila shaka yoyote.

11. Hakuna mmoja wenu anayetaka kumtawala mwenzake au kumkwamisha mwenzake kwenye mambo anayofanya.

12. Mnafanikiwa kwa wepesi zaidi mnapofanya kazi mkiwa pamoja kwa kuunganisha uwezo wa kazi na taaluma ya kila mmoja.

13. Kila mmoja ana malengo na mipango yake na kila mmoja anamuunga mkono mwenzake ili apate mafanikio anayoyatarajia.

14. Mnatatua matatizo yanayotokana na kutokuwa na muda, kutokuwa karibu na kila mmoja na mabadiliko ya aina yoyote ile kidogo kidogo na kwa uvumilivu wa hali ya juu kwa kila mmoja.

15. Kila mmoja anamfanya mwenzake ajiamini zaidi, mwenye mvuto, mwenye uhuru wa kufanya mambo yake na mwenye kuyafurahia maisha.

16. Hamfichani au kuwa na ajenda za siri. Kila mmoja anaweka wazi mambo yote kwa sababu mnajua kabisa kwa uzuri au ubaya, ni bora mwenza wako ajue ulivyo kwa kujiamini kabisa.

17. Kila mmoja anapenda mambo madogomadogo ambayo mwenza wake anayo.

18. Mnajaribu pamoja kufanya mambo mapya.

19. Kila mmoja anakubali anapokosea, bila aibu wala kujificha.

20. Kila mmoja anakuwa muwazi na kukubali kama jambo limemshinda au hawezi kulifanya.

21. Mnaelewa baadhi ya matatizo ya kimapenzi yanayowasumbua watu wengine na mnajitahidi kutofanya makosa wanayoyafanya wao.

Tazama dalili hizo na nyingine unazozijua kujiridhisha kama uwepo wa mwenza wako maishani mwako utadumu kwa muda mrefu kiasi gani. Jipime kama wewe pia unafanana na sifa kama hizo endapo mwenza wako akikuangalia anaweza kujiridhisha kwamba unavyo pia.

Toa Comment: Baada ya kusoma hii tunaomba tuachie maoni yako ili tupate mawazo yako kuhusu mada husika. Contact Us
Related Posts
COMMENT