Je Mahusiano Yako Yamevunjika na Unaumia ? Fanya Hivi

Songa mbele ! Mahusiano yako yamevunjika, siku, mwezi, miezi au mwaka. Ex wako amesha move on na anafurahia maisha na mwingine. Wewe bado uko busy kumuombea mabaya ili kwamba ajute kukuacha..kweli ? Hapana, wewe Songa mbele.

Haitajalisha ni kwa kiasi gani ulimpenda mtu na namna gani unavyojisikia vibaya kwa aliyokufanyia, jilazimishe kusahau na anza safari yako upya. Hakuna haja yoyote ya kumuombea mabaya.

Inatakiwa uelewe kuwa mahusiano yako yamefeli, kubaliana na hali hiyo, kama ni kuomba, omba Mungu akupe ujasiri wa kusonga mbele na kukupa moyo wa msamaha.

Ndio inauma sana, uliwekeza muda mwingi sana kwake, ulivumilia mengi na nia yako ilikua nzuri tu ya kuokoa mahusiano hayo. Ulifanya mambo ya msingi kabisa. Hivyo usijilaumu sana, unastahili kuwa na furaha.

Anza kufanyia kazi nafsi yako, jitathimini na anza upya. Maisha huwa hivyo, muda mwingine huja kwa namna ya kuumiza mno. Ila hatutapaswa kukata tamaa, hali unayopitia ni ya muda tu, hutabaki kama ulivyo!!! 


-T Hezron

#share na marafiki wapate somo pia.

Toa Comment: Baada ya kusoma hii tunaomba tuachie maoni yako ili tupate mawazo yako kuhusu mada husika. Contact Us
Related Posts
COMMENT