Hizi Sababu 10 za Wanawake Kuvutiwa Kimapenzi na Wanaume Wenye Uwezo Mkubwa Kiakili

1. Mwanamke akiwa na uwezo mkubwa kiakili, lazima atahitaji mwanaume anayeufikia au kuzidi uwezo huo ili waweze kujadiliana mambo mbalimbali.

2. Wanaume wenye akili sana hawazungumzii ngono wakati wote, wana mambo mengi sana ya kuzungumzia. Mwanamke mara zote huvutiwa sana na uwezo wa mwanaume kumudu mazungumzo ya kina kwa mada mbalimbali.

3. Wanawake wanapenda kuwa na mwanaume atakayevutiwa naye mara zote. Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili anavutia wanawake kirahisi sana.

4. Mvuto wa kingono unaazia akilini mwa mtu, mwanaume mwenye akili nyingi ana uwezo wa kuingia akilini mwa mwanamke mwenye uwezo mkubwa kiakili.

5. Uwezo mkubwa wa akili kwa mwanaume unaothibitisha kuwa unatafiti kutaka kujua na kujifunza mambo mbalimbali, njaa hiyo hiyo ya kutaka kujua mambo ndio atakayoionesha au atakayokuwa nayo kutaka kumjua mwanamke wake, vitu anavyothamini na pia katika kuujua mwili wa mwanamke wake. Mwanamke mwenye akili anapenda sana achunguzwe na mwanaume wake.

6. Mwanamke ni zaidi ya chombo cha kumstarehesha kingono mwanaume wake; bali ni kiumbe mwenye akili zake, mwenye imani, mwana jamii, mbunifu na kiumbe ambaye haeleweki kirahisi. Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili ana uwezo wa kuchunguza na kujua vitu vyote kuhusu mwanamke wake.

7. Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili ni chachu kubwa ya kufanikisha maendeleo ya kimaisha kwa mwanamke. Mwanamke anapenda kuwa na mwanaume ambaye anaweza kujifunza mengi kutoka kwake au watakaofanya maendeleo ya pamoja. Mwanamke akiwa na mwanaume wa aina hii atajikuta anapenda mara zote kuwa karibu na mwanaume wake. Atakubali starehe na shida zote watazozipata pamoja akiichukulia kama ni kutengeneza hadithi ya maisha yao.

8. Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili ambaye pia hana majivuno au kiburi ni rahisi kuishi naye, ni rahisi kufanya naye kazi na ni rahisi kuzungumza naye. Wanawake huwa wanasisimka wakiwa katika maongezi ya kimapenzi na mwanaume wa aina hii. Mhusishe mwanamke wako kwenye mazungumzo mazuri na yeye atakupatia mapenzi kwa kiwango kitakachokushangaza kabisa.

9. Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili anakuwa amepevuka kiasi kwamba uso wake, macho na muonekano wake wa nje tu unaweza kumuelezea alivyo. Mara nyingine jambo pekee unalotakiwa kufanya ni kumuangalia tu na yeye atapata hisia na ujumbe wa kutakwa kimapenzi na mwanaume wake.

10. Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili ana “kidunia chake” kila anapokuwepo. Anaingia sehemu akiwa anajiamini sana na uwepo wake lazima uonekane. Ni mtu imara mwenye akili thabiti inayojua mambo mengi. Akiwa karibu na mpenzi wake, mwanamke huyo mara moja atataka aendelee kuwepo sehemu hiyo.

Uwezo mkubwa wa kiakili unatokana na ukomavu wako tu, haijalishi kama una elimu za juu sana kama digrii ya chuo kikuu au PhD. Ni hali ya mtu kuwa na busara, kuwa na fikra kubwa, kuwathamini wanawake wote na kumuwezesha na kumuinua mwanamke pekee unayempenda maishani mwako.

Toa Comment: Baada ya kusoma hii tunaomba tuachie maoni yako ili tupate mawazo yako kuhusu mada husika. Contact Us
Related Posts
COMMENT